Tarehe 16 Disemba 2024, Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na wataalamu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mheshimiwa Erasto Mpete,wapo katika Manispaa ya Moshi kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Ziara hiyo inalenga kujifunza hasa katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato, usafi wa mazingira, na udhibiti wa taka.
Wakiwa makao makuu ya ofisi za Manispaa ya Moshi, wajumbe hao walipokelewa na Meya wa Manispaa ya Moshi Mhe.Zuberi Kidumo na baadaye kukaa na wataalamu wa Manispaa hiyo ambao waliwasilisha mada muhimu zinazohusiana na mafanikio ya manispaa hiyo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe