Jamii Halmashauri Mji Njombe mkoani Njombe imetakiwa kuzingatia malezi kwa watoto hasa katika kipindi hiki cha ukuaji wa sayansi na teknolojia .
Wito Huo umetolewa Mei 15 ,2024 na Ofisa Maendeleo Halmashauri ya mji Njombe Ndugu Enembora Lema alipokuwa akizungumza na Akinamama wa soko kuu la Njombe katika Siku ya Kimataifa ya familia Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 15, Mei.
Aliwaomba wazazi ma walezi kuhakikisha wanakuwa karibu katika ufuatiliaji wa mienendo ya watoto katika makuzi ilikuweza kujuwa tabia ambazo nihatarishi ziweze kulemewa kwa haraka .
Aidha ameiomba jamii kutoa taarifa pale vitendo viovu vinapotoke pasipo kivifumbia macho .
Maadhimisho ya siku ya familia kimataifa ya yalikuwa isemayo "Tukubali tofauti zetu kwenye Familia : Kuimarisha malezi ya Mtoto"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe