Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omari Januari 08,2024 alikutana na kufanya mazungumzo na watumishi wa kituo cha afya Makowo akiwataka kuzingatia miongozo mbalimbali katika utendaji wao wa kazi.
Bi. Judica amesema miongozo hiyo imewekwa ili ifuatwe na kusaidia kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima wakati wa utendaji kazi.
Aidha baada yakukagua miundombinu mbalimbali pamoja na vifaa katika kituo hicho ametoa rai kwa watumishi hao kuhakikisha wanakuwa walinzi wa vifaa hivyo na kutofumbia macho uovu wowote ikiwemo wizi wa vifaa tiba na dawa.
“Tufanye kazi kwa kufuata miongozo maovu yakitokea tusiyafumbie macho,tufanyie kazi kulingana na miongozo hata kama ni mtu anapatiwa onyo taratibu lazima zifuatwe,usione kitu kidogo ukakiacha ,usimamizi wa nidhamu bado upo pale.”Alisema Bi.Judica
Katika hatua nyingine amesisitiza suala la nidhamu ,ushirikiano,kujituma na uadilifu ili wananchi waendelee kuwa na imani na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya ambavyo Serikali imetoa gharama kubwa kuhakikisha huduma zinasogezwa karibu na wananchi.
Aidha amemtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe kufanya tathmini ya mahitaji wa watumishi na kufanya msawazo wa watumishi ili kila kituo kiwe na watumishi wanojitolesheleza kulingana na mahitaji.
Bi.Judica Omari alipata fursa yakuzungumza na watumishi hao baada ya kufanya ziara katika kituo hicho na kukagua miundombinu mbalimbali yakutolea huduma katika kituo hicho ikiwemo jengo la mama na mtoto,chumba cha upasuaji,jengo la kufulia ,jengo la kuhifadhia maiti na maabara ambayo yamekamilika na yatoa huduma pamoja na jengo la mionzi ambalo bado halijaanza kutoa huduma.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe