Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary awataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe kwenda kusimamia kwa ufanisi mkubwa wa utoaji wa chanjo Surua Rubela katika maeneo yao.
Bi Judica amesema hayo Februari 12,2023 kwenye Kikao cha Kamati ya Msingi (PHC) Kuhusu Dharura ya Magonjwa ya Mlipuko na Kampeni Shirikishi ya Surua ambapo katika kikao hicho kilicho wakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, taasissi binafsi na viongozi wadini.
Aidha amewaombwa Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi Pamoja na wataalamu wa afya kuhakikisha wanaenda kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa hatari wa surua kutokana hatari ambayo huweza pelekea mtoto ambaye hatapatiwa chanjo hiyo kuwa katika hali mbaya kiafya ambapo huweza pia sababisha maambukizi kwa wengine hivyo.
Akiendelea kuzungumza Katibu Tawala ametoa wito kwa kwa wataalamu kuimarisha usimamizi na utoaji huduma za chanjo kipindi chote cha kampeni na kutoa majibu ya kitaalamu haraka pale inapotokea upotoshaji ili kuweza kuepuka taarifa ambazo zinaleta taharuki katika jamii.
Katika kampeni hiyo ya kutokomeza ungonjwa Surua Rubela Mkoa wa Njombe wamepanga kuwafikia Watoto 94,343 kwa chanjo ya surua Rubella, ambapo kwa Halmashauri ya mji wa Njombe watoto 16,164 wanalengwa kufikiwa na chanjo hiyo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe