Halmashauri ya Mji Njombe kwa mwaka wa fedha 2016/17 ilipanga kukusanya na kutumia kiasi cha Shilingi 12, 214, 205,100 kwa ajili ya utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 10, 835, 160,100 ni ruzuku kutoka serikali kuu na Wahisani wa Maendeleo, na Shilingi 1, 379, 045,000 ni mapato ya ndani. Kwa ujumla hadi kufikia tarehe 30/6/2017, Halmashauri iliweza kupokea na kukusanya jumla ya Tsh. Sh. 9,960,776,540.52 sawa na 81.5% ya bajeti iliyoidhinishwa, ambapo kati ya fedha hizo Shilingi 8,740,141,438.28 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo toka Serikali kuu na shilingi 1,220,635,102.24 ni mapato ya ndani. Aidha, Halmshauri imepokea jumla ya Shilingi 260,093,173.24 nje ya bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa kampeni ya usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto chini ya miaka 5 (Birth Registration) na ruzuku ya utendaji wenye matokeo (P4R). Katika kipindi cha robo ya nne pekee halmashauri imeweza kupokea kiasi cha shilingi 3,266,103,966.45 (Ruzuku - 3,000,424,715.21 na mapato ya ndani - 265,679,251.24) kwa ajili ya miradi ya Maendeleo. Taarifa yake imeambatanishwa
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe