• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Jinsi ya kupata kibali cha ujenzi

Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi holela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.

UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI

  1. Kutimiza takwa la sheria ndogo za miji

  2. Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji wa jiji

  3. Kudhibiti ujenzi holela

TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI

Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Report submitted for Approval (RPA)”.

Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;

•Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector)

•Afisa Ardhi (Land Officer)

•Mpima  (Land Surveyor)

•Afisa Mipango Miji  (Town Planning Officer)

•Afisa Afya (Health and Sanitation Officer)

Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo;

  i.Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector) - kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications.

 ii. Afisa Ardhi (Land Officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.

 iii.Mpima wa Jiji (Land Surveyor) – kutambua mipaka halali

 iv. Afisa Mipango Miji wa Jiji (Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji, eneo la maegesho lipo, nk

 v. Afisa Afya (Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyema

Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali

Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya Halmashauri atakayopewa.

Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na Afisa mipango miji

MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI

• Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili (2) hadi manne (4)

• Hii ni pamoja na kuwasilisha  ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.

WAJIBU WA MWANANCHI

• Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya mji kwa kibali kutoka Halmashauri

• Wakazi wote wa katikati ya mji wanapaswa kukarabati au kujenga nyumba za kwenda juu (maghorofa) tu.

• Hairuhusiwi kujenga au kukarabati nyumba za chini.

TAHADHARI

• Endapo mwananchi yoyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka Halmashauri, atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba (7)

• Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha, Halmashauri  itampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa Halmashauri  itabomoa  jengo husika na kumdai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji huo

• Wananchi wote wa  Mji wa Njombe wanashauriwa kuacha ujenzi holela kwa kufuata sheria ndogo za ujenzi na kupata kibali cha ujenzi


Matangazo

  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 15, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 KWA SHULE ZA SEKONDARI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 21, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWENYE ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE March 25, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 06, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KITUO CHA AFYA MAKOWO CHAKABIDHIWA VIFAA TIBA

    March 04, 2023
  • SERIKALI YASAINI MIKATABA YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

    March 03, 2023
  • DC NJOMBE AKABIDHIWA MRADI WA VYUMBA VYA MADARASA

    December 08, 2022
  • SHAMRA SHAMRA MIAKA 61 YA UHURU NJOMBE WAANZA KWA USAFI SOKO KUU

    December 05, 2022
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe