Ni ugeni wa Watoto kutoka katika Kituo cha kulelea Watoto Compassion ambao leo umefika katika Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe na kutoa shukrani kwa misaada mbalimbali ambayo Ofisi hiyo imekua ikiwasaidia katika kuishi na kuwapa mazingira bora ya kusoma wakiwa na mahitaji na vifaa vya Shuleni.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha salamu hizo Mkurugenzi wa Shirika la Compassion Njombe Lucia Mlowe amesema kuwa kwa kipindi cha takribani miaka 6 Halmashauri imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kituo hicho jambo ambalo limekuwa likileta faraja kubwa kwa watoto hao.
“Nimekuja hapa nikiwa nimeambatana na hawa watoto kwani tumekuwa tukiwapokea katika kituo chetu kupitia Ustawi wa Jamii. Hawa Watoto ni wa Serikali na kupitia Ofisi ya Mkurugenzi tumekuwa tukipata mahitaji kama vyakula,vifaa vya shuleni na mahitaji mbalimbali jambo ambalo limesaidi kutatua changamoto za uendeshaji wa Kituo. Tulitaka pia waweze kuona maendeleo ya watoto wanaowahudumia na kuwalea.”Alisema Mlowe Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea Watoto Compassion
Akizungumza kwa niaba ya Watoto hao James Mlowe mwanafunzi anayesoma Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Mpechi na analelewa katika Kituo hicho amesema kuwa wanamshukuru Mkurugenzi kwa misaada ambayo amekuwa akiwasaidia kila wakati na wameiomba Serikali wakati wanapomaliza shule za Msingi na Kupangiwa Shule za Sekondari za Karibu ili kuweza kupata huduma kwa urahisi.
Aidha wamemwomba Mkurugenzi kuendelea kutoa misaada kwao na kwa wengine ambao wanahitaji misaada, kwani fursa waliyoipata itawawezesha wao kuwa raia wema na wenye kuleta maendeleo katika Nchi.
Mnamo tarehe 1 mwezi wa saba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe aliweza kukabidhi vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 2 laki moja kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima vya Compassion, Imiliwaha na Don Bosco ambapo misaada hiyo ilihusisha magodoro,mafuta,sukari,mchele sabuni na vifaa vya Shuleni.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe