• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Halmashauri ya Mji Njombe Yatoa Mshindi wa Tatu Maonesho ya Nane Nane

Tarehe iliyowekwa: August 8th, 2019

Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa kutoa mshindi wa Kwanza Kimkoa na wa tatu Kikanda katika kundi la Wakulima kwenye maonyesho ya nane nane mwaka 2019 ambapo  Bi. Ajentina Mvile ameibuka kidedea na kujipatia fedha na cheti cha ushindi ambapo mgeni rasmi katika maonyesho hayo alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akizungumza mara baada ya  kuibuka mshindi  Bi Ajentina ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Itulike Kata ya Ramadhan Halmashauri ya Mji Njombe amesema kuwa mambo yaliyompeleka kuweza kufanikiwa na Kuibuka Mkulima yeye akijikita kwenye zao la parachichi  ni jitihada ambazo amekuwa akionesha katika kuzingatia mbinu za kilimo bora na chenye tija na kuhakikisha kuwa ushauri wa  wataalamu wa kilimo unafanyiwa kazi.

“Kilimo kinahitaji jitihada binafsi. Tulipoanza kujishughulisha na kulima parachichi watu wengi waliona kama ni kupoteza muda. Hii ni kutokana na kuwa hapo mwanzo parachichi halikuwa na thamani na hali ya soko haikuwa ya uhakika.Wengi hawakuona Kilimo cha parachichi kama ni kilimo chenye tija.”Alisema Ajentina

Aliongezea kusema” Kwa sasa soko ni la uhakikika na mara baada ya kuona parachichi limepata soko nje na ndani ya nchi kila mtu sasa analima parachichi. Soko lipo na faida ipo. Nawashauri wakulima kuwa tunapopata taarifa ya kitu Fulani tusidharau kwani huwezi jua manufaa yake mbeleni.”

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo na kukabidhi zawadi kwa Washindi amesisitiza jamii kuzingatia matumizi ya ulaji wa lishe bora ili kuwa na afya bora na kupamba na tatizo la utapiamlo ambapo kwa kiasi kikubwa mikoa ya nyanda za juu kusini ndio imekuwa yenye asilimia kubwa ya kiwango cha tatizo la utapiamlo.

“Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika maonyesho haya haswa kwenye upande wa  usindikaji.Ni vyema tukaona ni namna gani tunawawezesha wasindikaji hawa wadogo kupata alama  ya ubora (TBS). Viwanda vione ni kwa namna gani vitatumia malighafi za wakulima na wafugaji. Alisema Pinda

Aidha amewataka wakulima na wafugaji kuongeza jitihada za zana za kilimo  ikiwa ni matumizi ya mbolea,viuatilifu na maghala ya  kuhifadhia chakula ikienda sambamba na utafuataji wa masoko ya ndani na nje.






Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe