• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe Yatoa ya Moyoni,Ni kasi ya Utekelezaji Ilani katika Halmashauri ya Mji Njombe

Tarehe iliyowekwa: June 25th, 2021

Ni maneno yaliyozungumzwa wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe ikiongozwa na Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Edward Mgaya, ambapo imepongeza kasi na umakini uliopo katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuipongeza Halmashauri kwa kuweza kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kutoka mapato ya ndani pekee kuchangia  kwenye utekelezaji wa miradi hiyo.

Akitoa pongezi hizo Mgaya amesema kuwa Halmashauri imeweza kufanya mambo makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya CCM jambo linaloleta imani kwa Wananchi kwa Chama Chao na kuwajengea Heshima.

“Tumeweza kutembelea miradi katika Sekta ya Afya, Elimu na barabara. Lakini katika pita zetu unaona ni kwa jinsi  gani Wananchi walivyoandaliwa na wanavyojishughulisha na kilimo cha aina tofauti tofauti. Hii inaonyesha maandalizi makubwa yaliyopo katika kutengeneza misingi ya Kiuchumi kwa Wananchi.Lakini pia nyie mmekwenda mbali zaidi na kuweza kuboresha Sekta ya afya na elimu. Mmejenga Zahanati, Kituo cha Afya Makowo ni kituo kizuri, mmeweza kujenga madarasa ya kutosha katika Shule za Sekondari na Msingi na kuanzisha Shule mpya hii inaonyesha jinsi mlivyo wabunifu, mlivyo na umoja, mnafanya usimamizi na ufuatiliaji katika miradi. Hata akija mgeni hatuna wasiwasi miradi yetu inafurahisha.Niwapongeze sana” Alisema Mgaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa Halmashauri imeweka utaratibu wa kupeleka fedha katika maeneo ambayo Wananchi wanakua wameonesha nia kwa kuanzisha mradi na kufikia hatua ya boma ndipo Halmashauri huwapatia fedha kwa ajili ya kufanya ukamilishaji wa mradi husika.Bi Mwenda aliendelea kufafanua kuwa licha ya kuwa mbinu hiyo imepelekea ushindani katika Kata na kuibuka kwa miradi mingi kwenye Halmashauri yapo maeneo ambapo mwamko wa Wananchi kuchangia umekua ni mdogo kulinganisha na maeneo mengine katika Halmashauri.

“Tuna ujenzi wa shule tatu mpya za Msingi. Mjimwema,Kambarage na Magufuli lengo la miradi hii ni kupunguza msongamano wa Wanafunzi katika shule zetu.Halmashauri tumeweza kuchangia kupitia mapato ya ndani, tunawashukuru Wananchi kwa kuweza kutuchangia na Serikali pia imetoa fedha kufanikisha ujenzi wa Shule hizi mpya.

Akitoa ufafanuzi kuhusu uchangiaji wa miradi ya maendeleo Mgaya amesema kuwa kazi ya chama ni kuendeleea kuhamasisha jamii isonge mbele na amewataka Waheshimiwa Madiwani kufanya mikutano ya hadhara na kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kuchangia miradi ya mendeleo kwani hata Taifa lilianza na misingi ya ujamaa na kujitegemea.

Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya CCM Wilaya ya Njombe wamesema kuwa Licha ya Halmashauri kuendelea kuwekeza katika miradi ya Maendeleo na miradi mingi kuwa na thamani ya pesa isiyokuwa na maswali, ni vyema maeneo yenye miradi hiyo ikawekewa mipaka na hati za maeneo hayo ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe ambaye ni Diwani wa Kata ya Utalingolo Erasto Mpete amesema kuwa Halmashauri itaendelea kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika na amewashukuru Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuwapelekea Wananchi maendeleo na kuhakikisha kuwa yale yote yalioagizwa na kuelekezwa na Kamamti ya Siasa yatakwenda kutekelezwa ipasavyo.

Kamati ya siasa ya Wilaya ya Njombe kwa muda wa siku mbili imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Halmashauri ya Mji Njombe ambapo jumla ya miradi 16 iliweza kukaguliwa yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3 kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha ambapo miradi hiyo mingi ikiwa ipo katika hatua mbalimbali za umaliziaji na mingine ikiwa tayari inatumika.

 

 

 

 

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe