• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mapambano dhidi ya UKIMWI Njombe yaendelea

Tarehe iliyowekwa: May 17th, 2019

Wakijadili mafanikio na changamoto za mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,  Wadau na Asasi zinazojishughulisha na   mapambano hayo katika Halmashauri ya Mji Njombe  wameazimia kwa pamoja kuendelea kuweka jitihada katika  kuelimisha jamii kuhusu janga la UKIMWI na kuitaka jamii kubadilika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mapambano dhidi  ya UKIMWI  katika Halmashauri ya Mji  Njombe, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga alisema kuwa elimu zaidi iendelee kutolewa hususani kwa wanafunzi mashuleni ili kuweza kunusuru kizazi cha sasa na kijacho dhidi ya janga hili.

“Tuna jukumu kubwa la kuendelea kuielimisha jamii bila kukata tamaa. Hatuna budi kama wadau kutumia fursa ya majukwaa  mbalimbali kuweza kuzungumzia swala la UKIMWI hususani katika Halmashauri yetu ambayo iko ndani ya Mkoa wa Njombe na unaongoza Kitaifa kwa kuwa na  asilimia 11.4. Katika sekta ya elimu tuone ni kwa namna gani tunaweza kuandaa nyimbo za mapambano dhidi ya UKIMWI wanafunzi wakawa wanaimba kama vile wanavyoimba nyimbo za shule hii itasaidi  kukuza uelewa na kutengeneza kizazi kitakachoweza kujikinga na janga la UKIMWI.”Alisema Luoga.

Aidha Luoga aliwataka Maafisa Elimu, Waratibu Elimu, Wakuu wa Shule na Waalimu Wakuu kutojiweka pembeni kwenye mapambano haya kwani wapo wanafunzi wengi ambao ni walengwa (wanaishi na VVU)  na wanapaswa kuangaliwa kwa kipekee  kwani Uwingi wa VVU kwa wanafunzi hawa umeonekana kuwa wa juu zaidi ambapo kiwango kinachotakiwa (copies kuwa juu ya 1000), kuepuka unyanyapaa lakini pia waalimu ndio wenye jukumu la kuhakikisha ratiba zinakuwa rafiki kwa wanafunzi wanaoenda kuchukua dawa lakini pia kwenye usimamizi wa matumizi ya dawa hizo haswa kwa wale waliopo shule za bweni.

Silverius  Kesanta mwakilishi kutoka shirika la Jhpiego AIDS Free ambalo linajihusisha na utoaji wa huduma za tohara ya hiari kwa wanaume ambaye  kwa upande wake alisema kuwa changamoto kubwa  inayowakabili ni uwepo wa watoa huduma wachache waliopatiwa mafunzo ya utoaji tohara ambao wamekuwa wakichukuliwa na Wizara kwenda kufanya kazi katika Mikoa mingine inayoendesha kampeni za Tohara pasipo na taarifa na hivyo kusitisha huduma katika vituo vyao vya kazi jambo linalopeleka kukoma kwa huduma katika maeneo yao ya awali.

Hata hivyo Silverius ameiomba  Halmashauri  kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha   huduma za tohara ikiwa ni miongoni mwa afua za mapambano dhidi ya UKIMWI na kuweza kumiliki huduma za tohara na kuondokana na mtazamo wa kuona swala la Tohara ni kwa ajili ya Asasi pekee.

Mwakilishi wa shirika la JSI Clarence Mkoba  alisema kuwa miongoni mwa mafanikio waliyoweza kufikia ni kuzijengea uwezo kamati za Kuthibiti UKIMWI kuhusu mwongozo wa usimamizi wa kamati hizo ambapo katika Halmashauri ya Mji Njombe wamefanikiwa kujengea uwezo Kata 05  kati ya 13 ambapo kumekuwa na mafanikio chanya.

Kwa upande wake  Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Mji Njombe Daniel Mwasongwe amesema kuwa warsha hizo ambazo zimekuwa zikifanyika kila kipindi cha robo mwaka zimekuwa na manufaa makubwa kwani zimesaidia upatikanaji wa taarifa za shughuli za utekelezaji wa Asasi.

“Kupitia warsha hizi tumekuwa tukibadilishana uzoefu,kupata taarifa za shughuli za utekelezaji  na kuweza kutatua changamoto kwa pamoja kwa jinsi kila mtu anavyofanya kazi katika kwenye mipaka yake. Usimamizi wa rasilimali kwa upande wa Halmashauri  unakuwa mzuri kwani kama kazi ipo kwenye mpango na inafanywa na Asasi fulani hakuna haja ya kutumia rasilimali kufanya kazi ambayo inafanywa na mdau mwingine. Hii pia inasaidia kuepusha migongano ya kazi kufanywa na asasi zaidi ya moja.”Alisema Daniel.

Daniel pia aliendelea kusema kuwa ni jukumu la jamii kuendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya ARV kwa WAVIU lengo ikiwa ni kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Ikumbukwe kuwa dira ya Taifa ya mapambano dhidi ya UKIMWI Tanzania ni kuwa na jamii isiyokuwa na maambukizi mapya ya VVU,Wakati mkakati wa dunia kwenye masuala ya VVU na UKIMWI ni kuwa Ifikapo 2030,dunia nzima inatakiwa kufika sifuri tatu(3 zero) yaani Maambukizi mapya ya VVU-0,Vifo vitokanavyo na UKIMWI-0,Unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU-(0) na malengo ya muda mfupi ikiwa Ifikapo 2020,dunia nzima inatakiwa kufikai asilimia tisini tatu (90%,90%90%),yaani 90% ya watu wote walioambukizwa VVU wajue hali zao (Wapime VVU), 90% ya watu waliokutwa na VVU wajiunge na huduma ART (Waanze  kutumia dawa), 90% ya wanaotumia dawa wawe wamefikia hali ya kufubaza VVU(Viral Load Seppression).

Halmashauri ya Mji Njombe imekuwa ikishirikiana na asasi mbalimbali ikiwemo HHU, JSI, SAUTI, AIDS FREE, COCODA, TULONGE AFYA, DREAM, CUAM, SECO, KIZAZI KIPYA, SHISO, BORESHA AFYA na  AGAPE kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe