Nyumba 6 zimeezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Njombe na kusababisha maafa kwa familia 6 katika kijiji cha Ikisa kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji Njombe.
Wakizungumza mara baada ya tukio hilo Wananchi waliofikwa na maafa hayo wamesema kuwa licha ya kutokea kwa maafa hayo hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa katika tukio hilo.
Akizungumza wakati alipowatembelea wahanga wa maafa hayo Katibu wa Mbunge Jimbo la Njombe Mjini Andreas Mahali amesema “"Tumefika hapa ili kuwashika mkono wahanga wa tukio hili la upepo kuezua nyumba tumekubaliana na Diwani wa kata hii kuwa baada ya kikao cha tathimini,Ofisi ya mbunge itarudi tena hapa kutoa msaada kwa familia hizi" Alisema
Jackan Mtewele ni Diwani wa Kata ya Uwemba ambaye anasema kuwa kwa sasa familia zilizopatwa na maafa hayo zimeifadhiwa kwa ndugu na jamaa wa karibu huku taratibu za kujenga makazi yao na kufanya ukarabati zikiendelea.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe