• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mwenge wa Uhuru Wamulika Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 6.2 Halmashauri ya Mji Njombe

Tarehe iliyowekwa: September 19th, 2019

Jumla ya Miradi tisa yenye thamani ya zaidi shilingi bilioni sita imekaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi  na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru  Septemba 18, 2019 katika Halmashauri ya Mji Njombe na kubainika kutokuwa na dosari katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa shughuli za ujenzi unaoendelea wa soko la kisasa Njombe, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ally ameipongeza Halmashauri ya Mji Njombe kwa kusimamia kwa uadilifu miradi hiyo na  kuitaka Halmashauri kuendelea na usimamizi huo madhubuti katika utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa  katika Halmashauri .

“Tungesema tuitishe harambee kiasi hiki cha bilioni tisa kisingeweza kukamilika kwa wakati. Mheshimiwa Rais amehakikisha anaweza kuleta fedha hizi za ujenzi wa soko ili Wananchi waweze kunufaika. Tuendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kazi anazofanya.Niwapongeze pia Wataalamu kwa kazi ya uaminifu, kazi iliyotukuka ni jambo jema sana. Niwaombe mkamilishe ujenzi wa soko hili kwa wakati lakini wale watakaopewa vizimba katika soko hili basi wafikiriwe wale watu ambao hali zao ni wanyonge. Wasitokee vigogo wakachukua vizimba halafu wao wanapangisha kwa watu wengine.”Alisema Mzee Mkongea Ally.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Edward  Franz  Mwalongo  Alisema  kuwa  Ujenzi  Wa  Soko  Hilo  Umeanza  Mwaka  2018   Kwa ajili  Ya  Kutoa  Huduma  Kwa  Wananchi  Wa  Mkoa  Wa  Njombe  Unaotarajia Kukamilishwa  Mwezi  Ujao Na  Kumuomba  Kiongozi  Wa  Mbio  Za  Mwenge  Kupeleka  Shukurani  Kwa  Rais  Wa  Jamhuri  Ya  Muungano  Wa  Tanzania Dkt  John  Pombe  Magufuli.

“Ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Rais Magufuli tumeweza kupata soko la kisasa Njombe, Mwenyewe umeona picha za awali kabla ya ujenzi wa soko hili.Soko hili likikamilika litakuwa ndio jengo litakalobeba sura ya mji wa njombe linataraji kuwa na Wafanyabiashara zaidi ya 700 jambo ambalo litakuza uchumi wa Wakazi wa Njombe na kitakuwa chanzo kikubwa cha mapato cha Halmashauri.

Naye Mkuu  Wa  Wilaya  Ya  Njombe  Bi. Ruth  Msafiri  Akizungumza  Kabla  Ya  Kwenda Kukabidhi  Mwenge  Wa  Uhuru  Katika   Wilaya  Ya  Makete  Ametaja  Takwimu  Ya  Maambukizi  Ya  Virusi  Vya  UKIMWI  Kupungua  Kwa  Wanaume  Kwani  Kati  Ya  Watu  147  Waliopima  Kwenye  Mkesha  Wa  Mwenge Wanawake wakiwa 46 na Wanaume 101,  Ni  Watu  5  Wanawake  Wawili  Na  Wanaume  Watatu  walibainika kuwa na maambukizi  mapya  ya UKIMWI.

“Kwa mara ya kwanza wanaume wamejitokeza kwa wingi kupima. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani Kampeni ya Pimba, Jitambue Ishi ilivyokuwa na manufaa” Ruth Msafiri alisema

Halmashauri  Ya  Mji  Wa  Njombe  Inaendelea  Na  Jitihada  Za  Kutekeleza  Malengo   Matano Ya  Darubini   Ya  Dira  Ya  Taifa   Ya  Maendeleo  Mwaka 2025  Ikiwemo  Lengo  Namba  Moja  La  Dira  Ya  Taifa La  Kuboresha  Hali  Ya  Maisha  Ya  Watanzania.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe