• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Naibu Waziri TAMISEMI apongeza ujenzi wa miradi ya Afya na Elimu Halmashauri ya Mji Njombe

Tarehe iliyowekwa: July 23rd, 2019

Naibu Waziri wa TAMISEMI  Mwita Waitara amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Njombe kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Makowo na Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Msingi Makowo Kata ya Makowo na shule ya Msingi Kambarage zilizopo Halmashauri ya Mji Njombe ambapo serikali imetoa zaidi ya Tsh. Milioni 72.5 kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hizo na kufurahishwa na hatua za ujenzi zinazoendelea huku akiipongeza  Halmashauri na Wananchi kwa ujumla kwa kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya hiyo.

“Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuanzisha, kuboresha na kusimamia miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa kero za wananchi zinatatuliwa. Zipo Halmashauri ambazo zimekuwa zikitekeleza miradi ya maendeleo hewa. Fedha zinapelekwa katika maeneo husika lakini miradi haipo. Wakati mwingine mradi haulingani na thamani ya fedha iliyotumika. Serikali ilishatoa maelekezo kuwa fedha zinazopelekwa kwa wananchi zitumike kwa malengo ya miradi husika na ndio maana leo nimepita ili niweze kukagua na kujiridhisha. Ninayozungumza hapa si ya kwangu ni maelekezo ya Serikali na tunafanya kazi kwa niaba ya Rais lazima yale tunayofanya yaendane na matamanio na Falsafa ya Mheshimiwa Rais” Alisema Waitara

Waitara amesema kuwa Halmashauri zinapaswa kuhakikisha kuwa asilimia 40 iliyotolewa maelekezo kutumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo inatumika ipasavyo na inapelekwa kutekeleza miradi husika na kutaka uwazi na uwajibikaji uzingatiwe katika kila hatua.

Awali akizungumza na Watumishi kutoka katika Halmashauri ya Mji Makambako, Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Waitara amewataka watumishi kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni za Utumishi wa umma huku akiwataka Watumishi kuwatembelea na kutoa huduma kwa Wananchi katika maeneo yao kwa kutoka ofisini.

Aidha, katika hali isiyo ya kawaida Wananchi wa Kata hiyo wameipongeza Serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikizichukuwa za  kuleta maendeleo na kuhakikisha kuwa viongozi wanawafikia Wananchi hata katika maeneo ya vijijini  na  Kumpongeza Naibu Waziri Waitara kwani ameweza kuvunja rekodi ya kuwa Naibu Waziri wa Kwanza kufika katika Kijiji hicho katika maisha yao yote Kijijini hapo.

“Katika maisha yetu yote hatujawahi kupokea ugeni kama huu. Wewe ni Naibu Waziri wa kwanza kufika katika Kata hii umevunja   rekodi, kwa kweli tumefarijika sana” Alisema Diwani wa Makowo Mhe. Mgaya.

Ziara ya Waitara inaendelea leo kwa kutembelea Halmashauri ya Ludewa na Makete katika Mkoa wa Njombe.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe