• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

RC Njombe akagua maendeleo ya stendi mpya na ujenzi wa soko la kisasa

Tarehe iliyowekwa: May 25th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amefanya ziara na kukagua shughuli za umaliziaji wa ujenzi stendi kuu mpya  iliyoanza kazi rasmi 11 Mei 2019  na kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa soko kuu la kisasa na kuridhishwa na kasi na viwango  vya ujenzi wa soko hilo.

Ziara hiyo iliyolenga kutambua na kupatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi mara baada ya kuanza rasmi kwa stendi kuu mpya, na  kuangalia thamani ya pesa iliyotumika katika hatua zinazoendelea za ujenzi wa soko kuu Njombe, ilijumuisha wajumbe wa  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.

Akizungumza na Wasafiri, Wajasiriamali wadogo, Mama Ntilie na Wadau mbalimbali wa usafirishaji na Wananchi kwa ujumla waliokuwepo katika eneo hilo la stendi, ambao wengi walipongeza jitihada za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuonekana kufurahishwa kuhamia katika stendi hiyo mpya, Sendeka amewataka Wananchi hao kuendelea kuiunga mkono na kuipongeza Serikali ya Dkt John Pombe Joseph Magufuli  ambayo imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa  miradi mikubwa na yenye tija kwa wananchi wa hali ya chini na wanyonge.

Mmoja wa Wajasiriamali wa bidhaa za vinywaji Mjini hapo John Msemwa alisema kuwa kero yake kubwa ni kuzuiwa kwa wao kuingia katika stendi hiyo kufanya biashara licha ya kuwa na kitambulisho cha Mhe. Rais jambo ambalo halikuwepo katika stendi ya zamani na linawakosesha wao kupata riziki.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo Sendeka amewataka Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo stendi ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji na kwamba utaratibu rasmi utaandaliwa kwa ajili ya matumizi ya stendi hiyo.

“Tupo katika hatua za mwisho za umaliziaji wa stendi. Ninachotaka niwahakikishieni ni kwamba Vitambulisho vya Mhe. Rais vitaheshimiwa kama ambavyo mwenyewe ameelekeza.Tutakaa na Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na baadaye tutakaa na ninyi ili kuweka utaratibu ambao utakuwa, rafiki, shirikishi na wa uwazi kwa Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wadau wa usafirishaji na watumiaji wote  wa stendi. Tukumbuke pia hatuwezi kuingiza  Mji Mzima stendi kufanya shughuli zao. Alisema Sendeka.

Akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za upatikanaji wa vibanda kwa ajili ya shughuli za biashara katika stendi kuu mpya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amemuhakikishai Mkuu wa Mkoa na kumtoa hofu kuwa Halmashauri ilifuata na inaendelea kufuata taratibu zote za manunuzi katika ukodishaji wa rasilimali za stendi mpya na mchakato wa manunuzi unaendelea kulingana na sheria kanuni na taratibu  na kumthibitishia  kupeleka nyaraka  zote za masuala ya manunuzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama alivyoagiza kwa  ajili ya kwenda kuzipitia na kujiridhisha na vyombo vya usalama kama taratibu zote za  manunuzi zimefuatwa ipasavyo.

Katika hatu nyingine Ole Sendeka ameipongeza Halmashauri na Mkandarasi Nandra Construction kwa kazi nzuri  yenye kasi na ubora ya  ujenzi wa soko la kisasa Njombe na amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anamaliza kazi hiyo kufikia Octoba 2019 kwa mujibu wa muda wa nyongeza waliiomba na amesema kuwa kwa kasi na shughuli zilizosalia ana imani kubwa muda uliobaki  unatosha kumaliza shughuli zilizobaki na soko kuanza kazi mara moja.

Halmashauri ya Mji Njombe inatekeleza mradi wa Ujenzi wa stendi ya kisasa  ambayo imeanza kutumika na mradi wa ujenzi wa soko la kisasa kupitia programu ya uboreshaji na uimarisha Miji ULGSP ambapo  kila mradi unatarajiwa kugharimu zaidi ya Bilioni 9 mpaka kukamilika kwake.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe