Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth msafiri amewataka wafanyabiashara wote wanaofanya biashara ya kuuza mali mbichi katika maeneo yasiyo rasmi ikiwa ni barabarani na kwenye magari kuwa ifikapo tarehe 08/03/2021 watu hao wao wameondoka kwenye maeneo hayo na watakaokiukwa watakamatwa na kuchukiliwa hatua kwani Halmashauri ya Mji Nombe ina maeneo mengi na masoko ya kufanyia biashara. Hayo yalisemwa katika kikao cha ushauri cha Wilaya kilichowahusisha wadau wa maendeleo lengo ikiwa kujadili rasimu ya bajeti kwa mwaka 2021/2022.
‘Hatuitaji kufanya biashara nje ya maeneo rasmi.Kwa soko jipya tunanguvu ya kutosha hatuhitaji watu kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi.Hatuwezi kuruhusu watu kutoa biashara zao nyumbani na sokoni na kuja kuuzia barabarani .Hili halikubaliki tunamasoko ya kutosha na tunahitaji Mji wetu uendelee kuwa na rekodi ya usafi kama ilivyokuwa awali. Yapo pia magari yanayosimama na kununua mali mbichi barabarani nawasisitiza pia hayo sio masoko na mwisho ni tarehe 08/03/2021 mara baada ya muda huo kupita nitawakamata. Kwa wale wanaouuza matunda kwenye magari njooni na vibali kama vipo tuone ni nani aliowaruhusu kufanya biashara kwenye magari.”Alisema Mkuu wa Wilaya
Wakitoa ushauri wao kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Wilaya Edward Mgaya amesema kuwa ni vyema ardhi ya iliyokuwa eneo la NJODECO kuchukua jukumu la kuichukua na baadae kuweza kutumika kwa ajili ya shughuli za uwekezaji.Kuweka mipango mizuri ya kurejesha viwanda. Kurejesha miundombinu
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kwenye kikao hicho wameendelea kuipongeza Halmashauri kwa makusanyo mazuri na kuitaka Halmashauri kuweka mikakati na kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwemo kutenga maeneo ya kuegesha malori,maeneo ya magulina maeneo ya michezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa yapo mengi ambayo Halmashauri ilitamani kufanya katika bajeti lakini Halmashauri ilikuwa inatakeleza mradi wa soko, na kwa sasa imeanza kuangalia maeneo ya kuongeza mapato ikiwa ni sambamba na mali za eneo la NJODECO.
Mwenda ameendelea kusema kuwa mipango mizuri inaendelea kutekelezwa na Halmashauri ikiwa ni sambamba na kuanza ujenzi wa vituo vya afya Luponde na Mjimwema na kuboresha ujenzi wa kituo cha afya Mjimwema.
Halmashauri ya Mji Njombe imeendelea na utaratibu wa kufanya vikao vya Kisheria kwenye kupitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka 2021/2022.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe