Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mamongolo iliyopo kijiji cha Mamongolo kata ya Makowo kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho ,wamewalisha shukrani zao kupitia shairi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan baada yakuzinduliwa zahanati mpya ya kisasa katika kijiji hicho.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt.Jabil Juma ameishukuru Serikali kwa kuendele kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hususan katika sekta ya afya ambapo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Mji Njombe imepokea zaidi ya Bilioni 2 zilizotumika kujenga miundombinu mbalimbali sambamba na kununua vifaa tiba vya kisasa vya kutolea huduma.
Wananchi wazungumza ya moyoni kufuatia uzinduzi wa zahati mpya ya kijiji cha Momongolo kilichopo kata ya Makowo.Waeleza namna walivyokuwa na changamoto ya kufuata huduma za afya mbali na makazi yao.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe