Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Mji Njombe – Kibena, kuhakikisha anazingatia masharti ya mkataba na kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.Mhe. Sweda ametoa maelekezo hayo tarehe 19 Juni 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa sekta ya afya.Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Hammakop ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari imetoa jumla ya shilingi milioni 900 zilizoanza utekelezaji wa mradi huo.Hospitali ya Mji Njombe ni miongoni mwa kongwe nchini ambazo zimepatiwa fedha na Serikali kwa lengo la kuboresha miundombinu yake ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.Mhe. Sweda ameongeza kuwa utekelezaji mzuri wa mradi huo utaleta unafuu mkubwa kwa wananchi wa Njombe wanaotegemea hospitali hiyo kwa huduma za afya za msingi.
Shule mpya ya Msingi Lunyanywi itaongeza usalama kwa watoto na kuwapunguzia wanafunzi wanaotoka Lunyanywi na maeneo jirani zaidi ya km 9 za kutembea kuifuata elimu katika shule ya Msingi Mjimwema.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amewataka wafundi wanatekeleza mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Yakobi kuhakikisha wanakamilisha kwa ubora uleule walioanza nao.Akizungumza Juni 18, 2025, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwalo hilo, Mhe. Sweda amepongeza ubora wa kazi iliyofanyika hadi sasa, ambapo zaidi ya shilingi milioni 169 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri zimeshatumika kutekeleza mradi huo ambao uko kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe