KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE NDG.GABRIEL KULABA AMEZINDUA RASMI DAWATI LA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KATIKA KITUO KIKUU CHA MABASI NJOMBE.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Mji Njombe – Kibena, kuhakikisha anazingatia masharti ya mkataba na kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.Mhe. Sweda ametoa maelekezo hayo tarehe 19 Juni 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa sekta ya afya.Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Hammakop ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari imetoa jumla ya shilingi milioni 900 zilizoanza utekelezaji wa mradi huo.Hospitali ya Mji Njombe ni miongoni mwa kongwe nchini ambazo zimepatiwa fedha na Serikali kwa lengo la kuboresha miundombinu yake ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.Mhe. Sweda ameongeza kuwa utekelezaji mzuri wa mradi huo utaleta unafuu mkubwa kwa wananchi wa Njombe wanaotegemea hospitali hiyo kwa huduma za afya za msingi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe