Diwani wa Kata ya Kifanya, Mhe. Nolasco Mtewele, amesema kuwa wananchi wa kata hiyo sasa wamepata kile walichokitamani kwa muda mrefu, kituo cha afya chenye huduma kamili, ikiwemo jengo la kuhifadhia maiti (mortuary) ambalo tayari limekamilika na linaendelea kutoa huduma.Mhe. Mtewele ameeleza kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Kifanya, huku akitoa pongezi kwa serikali na wadau wote walioshiriki kufanikisha mradi huo.Kwa muda mrefu, wananchi wa kata ya kifanya na maeneo jirani walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa huduma ya uhifadhi wa miili, hali iliyolazimu baadhi kusafiri umbali wa kilomita 50 kuifikia Hospitali ya Mji Njombe Kibena.
Wananchi wa kijiji cha Mfereke walipatiwa elimu ya umiliki wa ardhi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za kijiji kwa lengo la kupeana taarifa za maendeleo ya kijiji pamoja na kuwajengea wananchi uelewa kuhusu masuala ya ardhi kama njia mojawapo ya kuimarisha maendeleo ya kijiji.Katika mkutano huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ardhi na Mipango miji H/Mji Njombe, Emmanuel Luhamba alitoa elimu kuhusu masuala ya ardhi ikiwemo umuhimu wa kupanga, kupima na kumiliki ardhi kisheria pamoja na faida zake kiuchumi na kijamii. Elimu hiyo imelenga kuwajengea uelewa wakazi wa Mfereke kuhusu matumizi bora ya ardhi na nafasi ya ardhi katika kuinua kipato chao.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bw. Robert Sanga, ametoa wito kwa watumishi wapya waliokuwa wakijitolea katika Kitengo cha Ardhi kuzingatia nidhamu na maadili ya kazi katika ajira zao mpya Serikalini.Bw. Sanga alitoa wito huo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyoandaliwa na Kitengo cha Ardhi, ikiwa ni sehemu ya pongezi na kutambua mchango wao katika kuleta maendeleo kwa Halmashauri ya Mji Njombe.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe