Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt.Jabil Juma ameishukuru Serikali kwa kuendele kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hususan katika sekta ya afya ambapo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Mji Njombe imepokea zaidi ya Bilioni 2 zilizotumika kujenga miundombinu mbalimbali sambamba na kununua vifaa tiba vya kisasa vya kutolea huduma.
Wananchi wazungumza ya moyoni kufuatia uzinduzi wa zahati mpya ya kijiji cha Momongolo kilichopo kata ya Makowo.Waeleza namna walivyokuwa na changamoto ya kufuata huduma za afya mbali na makazi yao.
Kata ya Mokowo iliyopo kilomita 90 kutoka Mji wa Njombe ni miongoni mwa kata ambazo wananchi wake walikuwa na kiu ya kufikiwa na huduma mbalimbali ambazo zimewezekana katika kipindi cha miaka 4 ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan .Miongoni mwa kazi kubwa zilizofanywa na Serikali katika kata hii ni pamoja na :Ujenzi wa kituo kipya cha Afya Makowo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 600,chenye vifaa tiba vya kisasa ikiwemo mashine ya kidijitali ya mionzi(X-Ray),gari jipya la wagonjwa na chumba chenye vifaa kwa jili kufanya upasuaji pamoja Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Makowo kwa shilingi milioni 583 ambayo ilikuwa ni kilio cha wananchi cha muda mrefu.Halmashauri ya Mji Njombe tunasema asante wananchi wamefikiwa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe