Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe. Kisa Gwakisa Kasongwa amempa siku nne mmiliki wa kampuni ya Chai ya DL Group kiwanda cha Luponde kuhakikisha analipa madai ya wafanyakazi wake wote ndani ya siku 4.
Ametoa agizo hilo Julai 02 ,2024 alipoyembelea kiwandani hapo nakuzunhumza na wananchi pamoja na wafanyakazi ambapo Mhe Kisaa Kasongwa kampuni hiyo haiwatendei haki watumishi wake kwani ni miezi minne wameganya kazi bila malipo.
“Nimekuja kuwasikiliza wananchi wangu ambao mmekuwa mkipaza sauti niombe muwe wavumilivu huku Serikali ikiwa inapambania maslahi yenu ,nampa siku 4 mmiliki wa kiwanda hiki kuhakikisha anawalipa wafanyakazi wake wote ambao wanawadai Pamoja na kuwalipa mafao yao ya NSSF” Alisema Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itakuja na suluhisho la kudumu kuhusu mwekezaji huyo.
Waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe wameshauriwa kuiga mfano kwa kuweka kitengo maalum cha huduma kwa watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) katika hospitali za Wilaya kama ilivyo katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena), ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Ushauri huo umetolewa Julai 1,2024 na Mkurugenzi wa huduma za Afya lishe na Ustawi wa Jamii akiwa ameambatana na timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) iliyofika hospitali mji wa Njombe(Kibena) ,kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya nakuona uwepo wa vyumba maalum vyenye vifaa vya kisasa kwa ajili yakuwahudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) na changamoto nyingine za afya.
Kitengo cha kuhudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) kipo ndani ya jengo la mama na mtoto lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 173.3 ,fedha iliuojumuisha michango ya wananchi ,fedha kutoka TASAF, fedha za mapato ya ndani na michango ya wadau wa maendeleo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe